Home Habari Beki mpya Yanga ampiga mkwara Kagere

Beki mpya Yanga ampiga mkwara Kagere

748
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

HUENDA yale mateso ya waliyopata mabeki waliyo wengi Ligi Kuu Tanzania Bara hayatakuwa hivyo kwa beki mpya wa Yanga, Ally Mtoni ‘Sonso’, anayedai hana straika anayemuhofia.

Beki huyo tayari, taarifa zinaeleza amesaini kwa Wanajangwani hao mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli ingawa mwenyewe amekuwa na kigugumizi akisisitiza mazungumzo yanaendelea.

Hata hivyo aliliambi DIMBA Jumatano kwamba akihudumu katika kikosi hicho msimu ujao hatakuwa na presha yeyote kutoka kwa mashabiki wala aina ya mpinzani wakiwamo mastraika wasumbufu.

“Kila kitu ni hatua mambo mazuri hayahitaji haraka, kuhusu kuhofia straika hatari kama ulivyomtaja hapo mfungaji bora Meddie Kagere, kwangu mimi hapana kikubwa ni ushirikiano tu wa wachezaji wenzangu,” alisema.

Sonso alikuwa chaguo la Yanga dirisha dogo la usajili Novemba mwaka jana lakini dili hilo halikutiki kwa nyota huyo ambaye anakipiga pia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Ikumbukwe Kagere ndiye aliyekuwa mwiba mchungu kwa mabeki kadhaa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika hivi karibuni akifunga jumla ya mabao 23 akivunja rekodi ya Amiss Tambwe wa Yanga ya mabao 21 misimu mitatu iliyopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here