Home Burudani BELLA AINGIA STUDIO NA MWANA FA NA AY

BELLA AINGIA STUDIO NA MWANA FA NA AY

6978
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE


MKALI wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella, anatarajia kuachia kolabo yake mpya ambayo amewashirikisha mastaa wa Bongofleva, Mwana Fa na Ay itakayokuwa mahususi kwa maharusi.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Bella alisema ameamua kuwapa shavu manguli hao kwenye muziki kutokana na ubora wa kazi zao.

Alisema ngoma hiyo itatoka wakati wowote baada ya kumaliza kazi na Werasson ambayo itatoka Jumatatu ijayo.

“Nimeamua kufanya kazi na mastaa hao kwa kuwa nawakubali sana..wamekaa kwenye gemu muda mrefu na bado wanafanya vizuri,” alisema Bella.

Aidha, aliongeza kuwa mbali na mastaa hao, pia anatarajia kutoa ngoma na msanii wa kike Malaika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here