SHARE
Benard Paul ‘Ben Pol’

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Benard Paul ‘Ben Pol’, juzi alifanikiwa kukonga nyoyo za mamia ya wakazi wa mkoani Dodoma wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Antony Mavunde, katika shoo maalumu ya kuadhimisha miaka mitano ya klabu Cap Town.

Nyimbo kama ‘Moyo Mashine’, Sofia, Sambaira, ule alioshirikishwa na msanii Darasa ziliupamba usiku huo na kumfanya Mavunde ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana kupagawa kwa furaha.

Kabla ya Ben kupanda, msanii Mr. Bluu naye alifanya yake jukwaani na kumfanya Waziri huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kuungana na mashabiki kupata burudani hiyo.

Sherehe hizo ambazo ziliambatana na utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora na wateja bora wa klabu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wake, Frank Ngonyani, alisema wamejipanga kwa mwaka 2017 kutoa huduma za kipekee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here