SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA wa R&B Bernard Poul, maarufu kama Ben Pol, amesema licha ya kusakamwa kuhusu lini atafunga ndoa na mpenzi wake wa sasa, Anerlisa, raia wa Kenya, amekiri kuwa mwaka huu kwake utakuwa na mabadiliko mengi kuhusu muziki wake na maisha ya kawaida.

Ben Pol, ambaye kwa sasa yupo katika mahusiano na mwanadada huyo tajiri raia wa Kenya, amesema anatamani sana maisha ya ndoa na anatarajia kutimiza ndoto zake wakati wowote.

“Kila mmoja anatamani kutimiza kile alichokiahidi, mimi mwaka huu nina mambo mengi ya kufanya, ikiwemo kwenye muziki wangu na maisha ya kawaida, ukiniuliza naoa lini nitakujibu muda wowote, nadhani hilo nalo ni moja ya mipango yangu kwa sasa,” alisema Ben Pol.

Kwa sasa Ben Pol ambaye tayari amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo, anafanya vyema na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Wakuone’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here