Home Burudani BEN POL: MASHABIKI WA ARUSHA WALINIDATISHA

BEN POL: MASHABIKI WA ARUSHA WALINIDATISHA

295
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE
MKALI wa muziki wa RnB, Benard Paul, maarufu kama ‘Ben Pol’, amesema upendo alioonyeshwa na mashabiki wake jijini Arusha ulimpagawisha kiasi cha kujikuta akijirusha wakati wa shoo ya fiesta.
Ben Pol amesema hii ni mara ya kwanza kwa mashabiki zake kuonyesha upendo uliopitiliza kwake na kujikuta akipata furaha iliyopitiliza na kujirusha kwao wakati akiwa anatumbuiza.
“Nilijirusha tu kwa mashabiki zangu na wao wakanidaka, sijawaza kama nitapoteza kitu kwa sababu kikubwa nimeangalia upendo walionionyesha na kama kuna kitu kimepotea nadhani kinanunulika,” alisema Ben Pol.
Ben Pol amesema hii ni mara ya pili kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta na mwaka huu amejipanga kuwapa watu vitu adimu ambayo hawakuwahi kuvipata.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here