Home Burudani Ben Pol: Sitoki kimapenzi na Snura

Ben Pol: Sitoki kimapenzi na Snura

550
0
SHARE

NA BEATRICE KAIZA

NYOTA anayefanya vema kwenye muziki wa kizazi kipya Tanzania, Bernard Paul maarufu kama Ben Pol, ambaye anatamba na wimbo wake wa Moyo Mashine amesema anatamani kuingia kwenye tasnia ya filamu.

Ben Pol mwenye uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba katika mahadhi ya R&B ameshatoa kazi mbalimbali zilizomfanya kupata umaarufu na kutambulika sehemu mbalimbali duniani. Miongoni mwa kazi hizo ni Sofia, Samboila, Maneno, Unanichora na nyingine nyingi.

Kuingia kwenye filamu

“Uwezo wa kufanya filamu ninao endapo fursa zitajitokeza pia kipaji ninacho kama nikishirikishwa au nikipata usimamizi mzuri, kucheza filamu ni ndoto yangu ya muda mrefu tangu nilipokuwa mtoto.

Kufunga ndoa mwakani

“Nina mpango wa kufunga ndoa mwakani na mpenzi wangu ambaye sipo tayari kumtaja kwa sasa, kumekuwa na maswali mengi kutoka sehemu mbalimbali kuwa ni lini nitafunga ndoa.

Kurudi shule

“Licha ya kuwa mwanamuziki mkubwa na umri wangu kuwa mkubwa bado napenda kusoma, muda wangu mwingi napenda kufuatilia mambo mbalimbali ikiwemo kusoma vitabu, kufuatilia taarifa za kijamii na matukio, afya na uchumi. Napenda zaidi kusoma ingawa sikufanikiwa kumaliza masomo yangu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), natarajia kurudi shule kwa mara nyingine ili nimalize miaka yangu miwili.

Maana ya jina la mtoto wake

“Nimebahatika kupata mtoto ambaye nilimpa jina la Mali kwa kumtakia mema na mafanikio katika maisha yake na maana asili ya jina hilo ni kuonyesha thamani. Mara nyingi majina yanaumba kwa hiyo mali ni njia ya kumtabiria mwanangu kuwa mtu tofauti na kwenye uwezo kuichumi.

Mahusiano yake na Snura

“Snura ni msanii mwezangu na ni rafiki yangu wa karibu sana,  kuhusu taarifa zilizoenea kwamba nina uhusiano naye wa kimapenzi si za kweli na kwamba ukaribu wetu ni kwa ajili ya kazi tu na si kitu kingine,’’ alisema Ben Pol.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here