SHARE

RAPPER Sho Madjozi  kutokea Afrika Kusini ameongezwa katika orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Mandela 100 Global Citizen Festival litakalofanyika Desemba 2,2018 kwenye uwanja wa FNB mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Inaelezwa kuwa tamasha hilo ni kwaajili ya kumbukumbu ya Miaka 100 ya Hayati Nelson Mandela, ambapo pesa zitakazopatikana katika Tamasha hilo zitawasaidia wananchi wa Afrika Kusini wanaoishi katika maisha magumu  Afrika Kusini.

Sho Madjozi ata-share stage moja na wasanii wakali kama Beyonce, Casper Nyovest, Wizkid, Tiwa Savage, Usher, Chris Martin, Eddie Veder, Femi Kuti, Ed Sheeran, Pharrell Williams, Jay Z, ikiwa tamasha hilo litaongozwa na Mwanadada Bonang Mateba .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here