Home Burudani Bieber, mkewe kuoana tena

Bieber, mkewe kuoana tena

2185
0
SHARE

LOS ANGELES, Marekani

PESA kitu kingine asikwambie mtu. Unajua kwanini? Justin Bieber na mkewe, Hailey Baldwin, wamepanga kufunga ndoa kwa mara nyingine, eti ile ya kwanza haikunoga!

Taarifa za uhakika zimenyetisha kuwa hii ya safari hii itakuwa kiboko, tofauti na ya mwishoni mwa mwaka jana waliyofunga kwa siri.
Hii ya safari hii, wamepanga iwe kubwa lakini ni bahati mbaya kweli kwa wadaku kwani wamepania kuweka ulinzi mkali, kwamba ni ndugu na marafiki tu watakaopata kadi ya mwaliko.

ìHailey analisghulikia hilo akiwa na mtaalamu. Wamepania kweli kweli,î kilisema chanzo kuliambia jarida la PEOPLE.

Huenda wawili hao wangekuwa wameshafanya hivyo mapema zaidi lakini Bieber alijikuta akisumbuliwa na tatizo la afya ya akili mwanzoni mwa mwaka huu, hivyo mipango yote kuwekwa kando.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here