SHARE

Tima Sikilo

PAZIA la ufunguzi wa michuano ya Gombero Cup kwa mara ya kwanza linatarajiwa kufunguliwa leo kwa mchezo kati ya Tameri dhidi ya Itungi FC katika Uwanja wa Gombero Magomeni.

Michuano hiyo ya soka la makaratasi ‘chandimu’ itashirikisha timu nane, zilizopangwa katika  makundi mawili.

Mratibu wa Kombe hilo,Said Mohammed ‘Pimpo’,amesema maandalizi yote yapo tayari  wanachosubiri kipyenga kupulizwa.

“Tayari kila timu imeshajua kundi lake na itacheza na nani, tunatarajia kuwa na kombe ambalo litakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu timu hizi nyingi zinajuana lakini pia kwa muda mrefu katika uwanja huu hakukuwa na ligi.

Bingwa wa mashindano atazawadiwa mbuzi wawili ambapo na kuzitaja timu shiriki ni Wabishi Talent, Migo Hood, Mizuna na Senegali. Nyingine ni Itungi, Paris Malala, Bangi 2 na Tameri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here