Home Habari Bocco amvuta mido Azam FC

Bocco amvuta mido Azam FC

969
0
SHARE

NA SAADA SALIM

KIUNGO mshambuliaji wa Mumias Sugar ya Kenya, Abdallah Hamisi, amesema kilichomrejesha nchini Tanzania ni baada ya kutamani kucheza timu moja na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.

Abdallah, aliyewahi kutakiwa na klabu ya Simba kipindi cha usajili mkubwa, kwa sasa yupo nchini akifanya majaribio Azam FC, kwa lengo la kusajiliwa.

Kiungo huyo raia wa Tanzania ameliambia DIMBA jijini jana kwamba, yuko nchini kwa ajili ya mapumziko, lakini akitafuta nafasi katika kikosi cha Azam FC.

“Nimemaliza mkataba na Mumias, niko free nikashawishika kuja kujaribu kupata nafasi Azam na kuwa karibu na mtu ambaye napenda kucheza naye timu mmoja (Bocco),” alisema.

Abdallah alisema Bocco ni mchezaji anayeweza kubadilisha matokeo muda wowote na kulifahamu vizuri goli hali ambayo ilikuwa ndoto yake kucheza na mchezaji huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here