Home Habari BOCCO, KINGUE KUWAVAA MBABANE

BOCCO, KINGUE KUWAVAA MBABANE

387
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA,

NYOTA wawili wa Azam, John Bocco pamoja na Stephane Kingue watakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kinachotarajiwa kuondoka leo kwenda nchini Swaziland, kuwavaa wapinzani wao, Mbabane Swallows mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Bocco na Kingue ambao awali walikuwa wanasumbuliwa na majeraha, kwa sasa wapo fiti na wamejumuishwa katika kikosi hicho kinachokwenda kupambana ili kulinda ushindi wao wa bao 1-0 walioupata nyumbani.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu hiyo, Jafar Idd, nyota hao wapo fiti na wataambatana na wenzao katika mchezo huo wa marudiano ambao kwa vyovyote watatakiwa kulazimisha sare yoyote au ushindi ili kusonga mbele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here