SHARE

NA MWANDISHI WETU

WACHEZAJI wawili wa kutumainiwa katika kikosi cha Simba, John Bocco na Asante Kwasi, ambao hawakusafiri na timu kwenda Mbeya kutokana na kuwa majeruhi, kwa sasa wako fiti kurejea mzigoni.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, alisema ataanza kuwatumia wachezaji hao katika mechi ijayo dhidi ya Coastal Union, itakayopigwa Mei 8, jijini Dar es Salaam.

“Bocco ni mchezaji muhimu, nimefurahi kusikia wako vizuri sasa, natarajia kuwatumia katika mechi ijayo tutakayocheza Dar dhidi ya Coastal Union.

Wakati Mbelgiji huyo akieleza matumaini ya kurejea kwa wachezaji hao, Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema kwamba beki wao, Paul Bukaba, aliyeumia katika mechi dhidi ya Mbeya City, atalazimika kukaa nje kwa muda wa wiki mbili kwa matibabu kabla ya kurejea dimbani.

Katika hatua nyingine, Aussems ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya straika wake chipukizi, Rashid Juma, kutokana na uwezo anaoonyesha katika mechi za ligi zinazoendelea.

“Nilivyomuamini na kumpa nafasi hakuwa hivi, naona anaongezeka kila siku, hili ni jambo zuri katika kikosi changu,” alisema Aussems.

Simba itaingia uwanjani leo kuivaa Prisons ikiwa katika kasi kubwa ya kuifukuzia Yanga baada ya kufikisha pointi 75 katika michezo 29 iliyocheza, huku Yanga ikiendelea kileleni kwa kuwa na pointi 80, baada ya kucheza michezo 34.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here