SHARE
NAHODHA wa timu ya Azam, John Bocco

NA JESSCA NANGAWE,

NAHODHA wa timu ya Azam, John Bocco, amesema timu yake ilistahili ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na inajipanga kuchukua kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Simba bao 1-0 kupitia kwa mchezaji wao, Himid Mao.

Bacco alisema kwa sasa wanageukia ubingwa wa Tanzania bara baada ya kuweka heshima visiwani na lengo lao ni kuhakikisha wanapigana kuibuka na ubingwa huo.

“Tumemaliza Mapinduzi kwa heshima kubwa, hii inatupa nguvu ya kupigana tena kuhakikisha tunaweka heshima nyingine kwenye Ligi Kuu,” alisema mshambuliaji huyo wa Azam.

Alisema wanaanza ligi kuu huku wakiheshimu kila timu watakayokutana nayo ili kuhakikisha hawapotezi mechi zozote za nyumbani na ugenini.

Azam yenye pointi 30 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, imerejea  Dar es Salaam tayari kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumanne ijayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here