Home Habari BOSI YANGA ACHUKUA FOMU BODI YA LIGI

BOSI YANGA ACHUKUA FOMU BODI YA LIGI

489
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 15, mwaka huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alilithibitishia DIMBA Jumatano kwamba, Sanga amechukua fomu na atapambana na mwenyekiti anayemaliza muda wake Ahmed Yahya.

“Kwa taarifa niliyonayo mpaka mchana wa leo (jana), ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga pamoja na yule wa Kagera Sugar, Ahmed Yahya ndio ambao wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi ya uenyekiti,” alisema Lucas.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa TFF na kufanikisha kuingia madarakani kwa Rais Wallence Karia pamoja na Makamu wake, Michael Wambura, baada ya uongozi wa Jamal Malinzi uliodumu kwa miaka minne kumalizika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here