Home Michezo Kimataifa BUFFON AMUAGA USAIN BOLT

BUFFON AMUAGA USAIN BOLT

410
0
SHARE

TURIN, Italia

MLINDA mlango mkongwe wa klabu ya Juventus, Gianluigi Buffon, ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, kumuaga mwanariadha anayetarajiwa kustaafu baada ya mbio za London kumalizika.

Bolt anatarajiwa kutundika viatu vyake baada ya kuweka rekodi kali kwenye riadha duniani.

Buffon aliandika ujumbe huu huku akiwa ameambatanisha na picha ya Bolt: “Kila hadithi ina mwisho wake. Na pale mwanzo unapokuwa wa kustaajabisha, hata mwisho wake inabidi uwe wa kukumbukwa.

“Binadamu mwenye kasi zaidi kwenye riadha umeamua kustaafu baada ya maisha yenye mafanikio katika mchezo huo.

“Haujawahi kusimama hata siku moja. Endelea kukimbia Bolt. Ili dunia iendelee kukutafuta ulipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here