Home Habari Cameroon walia kutoswa Afcon 2019

Cameroon walia kutoswa Afcon 2019

3840
0
SHARE

YOUNDE, Cameroon

SERIKALI ya Cameroon imesema uamuzi wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf), kuipokonya uenyeji wa fainali za Afcon 2019 si wa haki na ni unyanyasaji mkubwa.

Ijumaa ya wiki iliyopita, Caf walitangaza kuinyima Cameroon nafasi hiyo, sababu kubwa ikiwa ni kuchelewa kwa maandalizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni, mwakani.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, Serikali imesikitishwa na hatua hiyo akisema imechukuliwa haraka mno.

Si tu maandalizi ya kusuasua, pia hali ya usalama Kaskazini mwa Cameroon iliwatia wasiwasi wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Caf walipokutana Ijumaa kabla ya kuja na uamuzi huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Bakary aliongeza kuwa kunyang’anywa uenyeji wa fainali hizo hakutawafanya waache ujenzi wa viwanja uliokuwa ukiendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here