SHARE

NA SHARIFA MMASI aliyekuwa Comoro

SAFARI ya Yanga nchini Comoro, imemfaidisha nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kwani alipata fursa ya kukutana na baba yake mdogo aitwaye Nuru Haroub pamoja na binamu yake wanaoishi nchini humo.

Yanga ambao walitua nchini jana kutokea Comoro walikokwenda kucheza na wenyeji wao Ngaya de Mbe, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo katika mchezo huo, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Licha ya kwamba Yanga walifurahia ushindi huo mnono, lakini kwa nahodha huyo wa Wanajangwani hao, furaha yake ilikuwa mara dufu baada ya kukutana na ndugu zake hao ambapo kabla ya kuondoka hapa nchini, alishauriwa na wazazi wake kuhakikisha anafanya kila linalowezekana kukutana nao uso kwa uso.

Zoezi la kukutana na ndugu zake hao lilianza siku ya kwanza walipotua nchini Comoro, ambapo siku ya pili ndipo walipokutana uwanjani na siku ya tatu Cannavaro akakaribishwa nyumbani kwa ndugu hao wanaokaa Moroni Mtaa wa Itsandraa, sehemu ambayo alizikwa Sheikh mkubwa, Alhabib Omar bin Sumeit.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Cannavaro alikiri kukutana na ndugu zake baada ya mechi kuisha na kwamba walifurahi kuonana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here