Home Habari CANNAVARO AKUBALI YAISHE

CANNAVARO AKUBALI YAISHE

869
0
SHARE

NA SAADA SALIM,

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema kwamba hana kinyongo kwa kutopata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi chake kwa kuamini kwamba ushindani wa namba ndani ya kikosi hicho umekuwa mkubwa.

Akizungumza na DIMBA, Cannavaro amesisitiza kwamba hana shaka na wachezaji wanaocheza nafasi yake ndani ya Yanga na kwamba anachokiamini yeye ni ushindi wa timu kuliko jambo lingine lolote.

“Siwezi kulalamika nikianzishwa benchi kwani timu kwa sasa imesheheni vijana wenye uwezo mkubwa na sisi wote kwa pamoja tunataka Yanga ipate mafanikio.

“Kwangu mimi si kwamba kiwango changu kimeshuka bali ni ushindani tu wa namba, niweke bayana kuwa sina kinyongo chochote na nitaendelea kushirikiana na kila mmoja na pale nitakapopewa nafasi katika timu nitaitumia vizuri,” alisema.

Cannavaro amekutana na ushindani mkubwa wa namba katika kikosi cha timu hiyo kutokana na uwepo wa Kelvin Yondani, Vincent Bossou pamoja na Andrew Vincent na sasa ameweka bayana kuwa hana kinyongo chochote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here