SHARE

NA WINFRIDA MTOI

BEKI wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewatuliza mashabiki wa timu hiyo wanaomponda straika mpya wa kikosi hicho, David Molinga na kusema hawajui wachezaji wazuri.
Molinga alisajiliwa na Yanga msimu huu kutoka FC Lupopo ya DR Congo na mechi yake ya kwanza ya mashindano ilikuwa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.


Cannavaro alisema, anawashangaa watu wanaomuona Molinga kuwa ni mchezaji asiyekuwa na kiwango na kumhukumu kwa michezo michache.
Alisema,kama beki aliyewahi kukutana na washambuliaji tofauti, amemuangalia Molinga na kubaini ni bonge la mchezaji na atadhihirisha hilo huko mbele jinsi anavyoendelea kucheza.


“Eti watu wanasema Molinga si mchezaji mzuri, nawashangaa sana au wanataka hadi afunge mabao ndiyo wajue ni mchezaji, kwa naamini yule ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa mtamuona tu,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here