SHARE

NA BRIGHITER MASAKI

MSANII anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva, Careen Gardner ‘Malkia Careen’ ameweka wazi kuwa roho yake itatulia kama atafanya kazi na mwanamuziki maarufu wa dansi, Christian Bella.

Akizungumza na DIMBA Careen alisema,kila mwanamuziki anakuwa na ndoto za kufanya kazi na mtu anayempenda hivyo kwa upande wake anatamani kufanya na Christian Bella kwa kuwa anajuwa muziki na anaimba vizuri.

“Kwa kweli moyo wangu utafurahi sana siku nitamtia mikononi Christian Bella ndiyo ndoto yangu kubwa ya siku zote itakapotimia. Hata alipofanya kazi na Hamisa Mobeto kwa kweli nilipenda mno ila naamini ipo siku ndoto yangu itatimia kwa kufanya naye kazi” alisema Careen.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here