Home Habari CHAMA SAFI KUWAVAA LIPULI

CHAMA SAFI KUWAVAA LIPULI

2139
0
SHARE

NA SAADA SALIM


HABARI njema kwa mashabiki wa Simba ni kwamba, kibali cha Uhamisho wa Kimataifa (ITC) cha kiungo wao fundi, Clatous Chama, kimeshawasili na sasa ni ruksa kwake kuitumikia timu hiyo katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo huyo Mzambia amekosa michezo miwili dhidi ya Prisons, Wekundu hao wa Msimbazi wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 na ushindi mwingine wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City na sasa yupo tayari kuwavaa Lipuli FC katika mchezo unaofuata.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hajji Manara, alithibitisha kufika kwa kibali hicho juzi jioni na sasa Chama ni ruksa kuitumikia timu yake hiyo katika michezo inayokuja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here