SHARE

NEW YORK, Marekani
MKALI wa Hip-Hop, Chance the Rapper, amefanikiwa kuiachia albamu yake iliyosubiriwa kwa muda mrefu, ‘The Big Day’, aliyompa shavu pia mkongwe, Timbaland.

Albamu hiyo imeelezewa kuwa ni inayohusisha mambo ya kifamilia, kwani Chance amempa nafasi pia mdogo wake wa kiume, Taylor Bennett, ambaye ni msanii wa Hip-Hop.

Wengine ni Bon Iver, Benjamin Gibbard, Shawn Mendes, Murda Beatz pamoja na baba mzazi wa rapa Chance, Ken Bennett.

Kuibuka kwa albamu hiyo ya Chance kunakuja baada ya yeye mwenyewe kushirikishwa katika kazi za wababe kama DJ Khaled (‘I’m the One’) na ile ya ‘Don’t Cross Me’ iliyopo katika albamu ya ‘No .6 Collaborations Project’ ya Ed Sheeran.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here