SHARE

Na Lulu Ringo, Dar es S,alaam.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga raia wa Zimbabwe, Obrey Chirwa muda mfupi baada ya kusajiliwa na Azam Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja amesema atahakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu wa 2018/19.

Chirwa amesajiliwa na Azam akitokea klabu ya No-goom El Mostakbal Fotball ya nchini Misri.

“Nimekuja kupambana ili Azam ichukue ubingwa na itachukua kwasababu mimi nipo na uwezo wangu unajulikana Azam itachukua ubingwa na mengine mtayaona uwanjani,” amejinadi Chirwa mbele ya waandishi wa habari.

Awali Chirwa alielezwa kuja nchini kwa lengo la kusajiliwa tena na klabu yake ya zamani ya Yanga, baada ya ujumbe wa sauti aliowatumia Yanga kuomba kurejea klabuni hapo baada ya mambo kuwa magumu katika klabu aliyokwenda  kuitumikia huko Misri.

Katika sauti hiyo ya Chirwa yenye ujumbe kwa wachezaji wa yanga, amedai kutokulipwa pesa zake za usajili ndiyo maana ameamua kurudi. Siku kadhaa Chirwa alionekana akishuhudia mtanange wa Yanga dhidi ya Alliance mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Baada ya tetesi hizo kuvuma Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alijitokeza na kusema hana mpango na huduma ya mchezaji huyo kwakua hana uvumilivu na klabu wakati inapopitia kipindi kigumu kiuchumi.

Azam ndio timu inayoongoza Ligi kwa sasa ikiwa kileleni na jumla ya alama 30 tafauti ya alama 4 kwa Simba na Yanga wenye alama 26, Azam imeshinda michezo tisa imetoa sare michezo mitatu kati ya michezo 12 iliyocheza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here