SHARE

NA JESSCA NANGAWE                   |          


MWIMBAJI nguli wa muziki wa dansi nchini, ‘Kamarade’ Ally Choki, ameibuka na ngoma mpya inayoitwa ‘Noor’, ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wa jiji la Mwanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Wiki iliyopita Choki, ambaye ni mwimbaji wa zamani wa bendi ya Twanga Pepeta, alitambulishwa rasmi kujiunga na Super Kamanyola ya jijini Mwanza, ambapo huo ndio wimbo wake wa kwanza kuitungia bendi hiyo.

Akizungumza na DIMBA, Choki alisema wimbo huo ni maalumu pia kwa mashabiki wa Super Kamanyola, ambayo maskani yake ya kudumu ipo katika viwanja vya Villa Park.

Alisema wiki ijayo watauanzia mazoezi wimbo huo, ambao anaamini utawashika wadau wa muziki Kanda ya Ziwa, ambako ameamua kujichimbia ili kuwapa burudani ya nguvu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here