SHARE

NA JESSCA NANGAWE


HALI ya afya ya mwanamuziki gwiji wa dansi nchini, Kamarade Ally Choki, aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, imeanza kuimarika.

Akizungumza na DIMBA, kaka mkubwa wa Choki, Hamadi Choki, ambaye ndiye anayemuuguza mwanamuziki huyo wa zamani wa bendi za Twanga Pepeta na Extra Bongo, alisema afya ya mdogo wake inaimarika tofauti na alivyokuwa awali.

Alisema jana asubuhi mwanamuziki huyo alizungumzia maendeleo ya afya yake na kusema bado anaumwa, ingawa ameanza kujisikia mabadiliko na kuwaomba Watanzania wamuombee apone haraka.

“Naumwa kwakweli, ingawa nimeanza kupata nafuu lakini kubwa nawaomba Watanzania waendelee kuniombea nipone na kurudi upya jukwaani kuwapa burudani kutoka kwenye koo langu,” alinukuliwa Choki.

Kwa zaidi ya wiki sasa, Choki amelazwa katika Hospitali hiyo akiwa anasumbuliwa na maradhi ya sukari na presha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here