SHARE

LONDON, England

KUFUATIA ripoti kuwa Antonio Conte anataka kutimka darajani, klabu ya Chelsea imesisitiza kuwa kocha wao huyo bado ana furaha ndani ya klabu.

Mapema wiki hii iliripotiwa kuwa, Muitaliano huyo hakufurahishwa na jinsi klabu hiyo inavyokuwa nzito kukamilisha dili mbalimbali za usajili sokoni kuelekea msimu mpya, ambapo kocha huyo anatarajiwa kuwaongoza mabingwa hao wa Ligi Kuu England katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mtandao wa Sky Sports unaelewa kuwa, Chelsea wana imani na Conte, ambaye yuko mapumzikoni hivi sasa, ataendelea kuinoa timu hiyo na atarudi kwa ajili ya kuwaongoza vijana wake kwenye ‘pre-season’ ndani ya wiki ya kwanza ya mwezi Julai kama ilivyopangwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here