Home Michezo Kimataifa CONTE: BADO NIPO NIPO CHELSEA

CONTE: BADO NIPO NIPO CHELSEA

243
0
SHARE

LONDON, England

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, amesema kuwa ataendelea kuinoa timu hiyo msimu ujao na hana mpango wa kuhamia Inter Milan ya Italia kama vyombo vya habari barani Ulaya vinavyolihusisha jina lake na miamba hao.

Conte ameiongoza timu yake ya Chelsea kung’ang’ania kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi 11 na tetesi zilianza kuibuka kuwa huenda akatua Inter mwishoni mwa msimu huu lakini mshindi huyo wa tuzo ya kocha bora wa mwaka ya London alisema bado yupo yupo darajani.

“Matumaini yangu ni kuendelea kuwepo hapa (Chelsea) kwa miaka mingi. Nimeridhishwa na vijana wangu kwa sababu wamenionesha dhamira yao ya kupambana kwa ajili ya kushinda taji.

“Kitu cha muhimu ni mafanikio ya klabu, wachezaji na meneja. Na cha muhimu zaidi ni kuendelea kuwa hivi kwa sababu lolote linaweza kutokea, ila tunataka kuendelea kutesa kileleni.

“Nina wachezaji wenye uzoefu wa kushinda mataji na presha kama hizi,” alisema Conte.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here