SHARE

LONDON, England

LICHA ya kikosi chake kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi 14, kocha wa Chelsea, Antonio Conte, amedai kuwa Manchester United huenda ikanyakua ubingwa wa ligi hiyo kutokana na uimara wa kikosi chao.

United haijapoteza michezo 15 waliyocheza hadi sasa, ikitoa sare michezo mitatu kati ya minne ya mwisho na Conte alisisitiza kuwa kikosi hicho cha Jose Mourinho kitaendelea kuwapa upinzani wa hali ya juu kwenye mbio za ubingwa.

Conte ambaye kikosi chake kitaivaa Burnley leo kwenye dimba la Turf Moor, alisema: “Sikilizeni, zipo timu sita zenye nguvu na uwezo wa kupigania huu ubingwa, Man United pina naijumuisha hapo, wana kikosi kizuri.

“Kwa sasa ni makosa makubwa kufikiri kwamba tunalikaribia taji. Imebaki michezo 14 kwa timu zote, tukimaliza hiyo michezo vizuri tutakuwa na haki ya kusherehekea,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here