SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA mjasiriamali Faiza Ally amekiri kuwa maambukizi ya virusi vya Corona yameathiri biashara zake kwa kiasi kikubwa jambo linalomuweka kwenye wakati mgumu.

Faiza ambaye amekua akijishughulisha na biashara za kusafiri kuelekea China amedai tangu mwezi Januari hajaweza kufanya biashara yoyote hadi sasa.

ìKwa kweli ni ugonjwa unaotisha, kikubwa tuombeane ili uishe, kwa upande wangu kama mfanyabaishara nimeathirikia kwa kiasi kikubwa s ana, siwezi tena kusafiri kwenda China hadi hapo hali itakapokaa sawaîalisema Faiza.

Aidha Faiza alisema, anashukuru kusikia meneo mbalimbali nchini China ugonjwa huo ukiwa umepungua kusambaa na hivyo kumpa moyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here