SHARE

NA BRIGHITER MASAKI

MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ ameunga mkono jitihada za kupambana na janga la Corona kwa kugawa ndoo pamoja na sabuni kwa mama na baba lishe katika solo la Tegeta Nyuki na Bungu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Lulu alisema,tunapitia katika wakati mgumu kutokana na virusi vya corona hivyo kuwaomba watanzania kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya wanaotaka
watu kunawa na sabuni na maji ya kutiririka.

“Nikiwa na wenzangu tumeaamua kuwafikiria mama na baba lishe ambao wengi hawajawatazama, hivyo tumewapa vifaa vya kujikinga na Corona wanapokuwa kwenye biashara zao wao na wateja zao” alisema Lulu

“Nadhani wakati mwingine watu wanatamani kujikinga labda hawana vifaa watanzania wenye nacho tujitaidi kuwasaidia wasionacho kusaidia kujikinga na Corona” aliongeza Lulu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here