SHARE

NA TIMA SIKILO

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amekwama kurudi nchini kutokana na janga virusi vya ugonjwa wa corona linalosumbua dunia kwa sasa.

Eymael yuko mapumzikoni nchini Ubelgiji na alipanga kurudi jijini Dar es Salaam mapema mwezi huu lakini hali ya usafiri nchini humo imekuwa kikwazo kurejea nchini kuendelea na majukumu yake.

Eymael ambaye aliondoka mara baada ya Ligi kusimamishwa kutokana tahadhari ya ugonjwa corona,alisema, hali ya usafiri wa anga nchini humo ni ngumu kutokana na kuzuiwa kwa ndege kuingia na kutoka ili kuepusha kuongezeka kwa maambukizi.

Alisema, anajaribu kupambana aone kama anaweza kufanikiwa kupata tiketi ya ndege ili aweze kurudi Tanzania mapema lakini sio kazi rahisi hivyo kutaka mashabiki na viongozi wa Yanga wawe na subira.

Nipo salama na familia yangu lakini ninapambana kuhakikisha ninarudi huko nimekuwa nikiwasiliana na maagenti mbalimbali ili niweze kupata tiketi ya ndege kwa wakati huu lakini imekuwa ngumu hivyo naendelea kupambana kutafuta njia ya kurudi,îalisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here