Home Habari Coutinho aacha siri nzito Yanga

Coutinho aacha siri nzito Yanga

1260
0
SHARE

NA SALMA MPELI

KIUNGO wa zamani wa Yanga, Andrew Coutinho, ameondoka juzi jijini Dar es Salaam kurejea kwao nchini Brazil, lakini akiwa ameacha siri nzito ndani ya klabu hiyo, huku kukiwa na tetesi za kurejea kuitumikia timu yake hiyo ya zamani.

Mchezaji huyo alitua nchini mwishoni mwa wiki iliyopita na kuishuhudia timu yake hiyo ya zamani ikiumana na Majimaji FC, mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Ujio wa mchezaji huyo nchini unahusishwa na kurejea kwake kwenye klabu hiyo kutokana na kuletwa na mmoja wa mabosi wa Yanga na kufikia nyumbani kwake.

Coutinho kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Rakhine United, iliyokuwa inashiriki ligi kuu ya nchini Myanmar, ambayo aliisaidia kumaliza ligi ikishika nafasi ya 10, ikiwa na pointi 18.

Habari zilizothibitishwa na kiongozi mmoja mwandamizi ambaye hakupenda jina lake litajwe, zinadai kuwa Yanga ipo katika harakati za kumrejesha mchezaji huyo, huku ikiwa na mpango wa kumuacha mchezaji mmoja wa kigeni katika dirisha dogo la usajili.

Katika michuano hiyo, Coutinho aliifungia timu yake mabao 10 na kumaliza ikiwa nafasi hiyo katika Ligi hiyo iliyokuwa na timu 12 na mbili za mwisho ziliyaaga mashindano hayo kwa kushuka daraja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here