SHARE

MUNICH, UJERUMANI

KLABU ya Bayern Munich imefikia makubaliano na klabu ya FC Barcelona ya kumchukua nyota wa kimataifa wa Brazili , Philippe Coutinho kwa mkopo wa mwaka mzima huku kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja mkali huyo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Ujerumani , waliweka wazi usajili huo baada ya mchezo wao dhidi ya Hertha Berlin ambao uliisha kwa sare ya bao 2-2.

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazili, ambaye hakuwa na msimu mzuri Catalan, wakati wowote kuanzia sasa atatua nchini Munich kwaajili ya kukamilisha taratibu nyingine pamoja na kufanyiwa vipimo vya afya.

Mkurugenzi  mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge pamoja na mkurugenzi wa ufundi , Hasan Salihamidzic wiki hii walikuwa nchini Hispania, kukutana na viongozi wa Barcelona kukamilisha dili hilo.

“Nathibitisha kuwa Jumatano iliyopita nilikuwa na Hassan katika  Barcelona kufanya makubaliano ya klabu pamoja na mchezaji ,” aliongea hayo katika mtandao wa klabu hiyo.

Naye Salihamidzic, aliongeza kuwa pia naishukuru Barcelona, vitu vidogo tutaweza kuvimalizia lakini tunafuraha kwa kumleta mchezaji huyu Bayern.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here