Home Habari Coutinho kwenda PSG au Juve?

Coutinho kwenda PSG au Juve?

2481
0
SHARE

CATALUNYA, Hispania

TAYARI kiungo mshambuliaji wa Kibrazil, Philippe Coutinho, ameshawasilisha ombi la kuondoka klabuni hapo, kwa mujibu wa gazeti la Cadena Ser.

Hiyo inaziweka mkao wa kula klabu za PSG na Juventus, ambazo tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, zimekuwa zikimfukuzia.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool ndiyo kwanza ana mwaka mmoja Camp Nou lakini ameshindwa kufikia matarajio ya mabosi na mashabiki wake walioamini angeng’ara.

Kwa upande mwingine, taarifa ya kuondoka kwake Barca itazifurahisha klabu za Chelsea na Manchester United, ambazo pia zinaitaka huduma yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here