Home Michezo Kimataifa CURRY ASAINI MKATABA WA KUTISHA NBA

CURRY ASAINI MKATABA WA KUTISHA NBA

425
0
SHARE

CALIFORNIA, Marekani

MKALI wa kikapu anayekipiga katika  timu ya Golden State Warriors, Stephen Curry, amekubali kumwaga wino kwenye mkataba mnono wa kusalia ndani ya timu hiyo, mkataba unaotajwa kuwa wa thamani sana katika historia ya NBA.

Curry alikubali kuongeza mkataba huo utakaomfanya akitumikie kikosi cha mabingwa hao hadi mwaka 2022 na ni mkataba wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 201, mkataba uliovunja rekodi ya mkataba wa awali aliousaini wenye thamani ya dola milioni 200.

Katika kipindi cha miaka nane ya kucheza mpira wa kikapu NBA, Mmarekani huyo amedumu na timu moja tu ya Warriors na alishinda taji lake la pili ndani ya miaka mitatu Juni, akimpiku LeBron James wa Cleveland Cavaliers.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here