SHARE

NEW YORK, Marekani

UJAUZITO wa mcheza tenisi namba moja duniani, Serena Williams, utamsababisha akose michuano mikubwa mitatu hivyo kumfanya ashuke katika chati za ubora, imebainika.

Mapema wiki hii, Serena alijitokeza katika mitandao ya kijamii na kukiri kuwa ni mjamzito.

Mwanadada huyo mwenye mika 35, aliweka picha yake kwenye mtandao wa snapchat akiwa amejipiga picha kwenye kioo na kuandika ‘20 weeks’ yaani majuma 20 kisha akaifuta hiyo post.

Iwapo itathibitika kwa hakika kuwa ni mjamzito, Serena anaweza kuzikosa Grans Slams tatu yaani French Open, Wimbledon na US Open.

Nyota huyo wa tenisi Marekani amekuwa katika mahusiano kwa miezi 15 na mchumba wake, Alexis Ohanian, mmiliki wa Reddit waliochumbiana Desemba mwaka jana.

Serena (35) alitegemea kurejea katika namba moja ya ubora wa tenisi wiki ijayo, lakini kwa hali yake ya sasa itamlazimisha kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima pamoja na kukosa mashindano ya Wimbledon.

Hiyo inamaanisha kwamba, atashindwa kutetea taji lake la Wimbledon alilotwaa mwaka jana baada ya kumshinda Angelique Kerber kwa seti 7-5, 6-3.

Pia inaonyesha kwamba, Serena alikuwa mjamzito wakati aliposhinda taji la 23 la Grand Slam la mashindano ya Australian Open mwezi Januari mwaka huu.

Serena ambaye wiki ijayo atakuwa mchezaji namba moja, atabaki katika nafasi yake kwa mujibu wa sheria WTA, kama atakuwa tayari kurejea uwanjani na kushiriki mashindano ndani ya miezi 12 baada ya kujifungua.

Hata hivyo, picha yake hiyo aliiondoa haraka mtandaoni, lakini wawakilishi wake baadaye walithibitisha ujauzito huo.

Waandaaji wa mashindano ya tenisi ya US Open walimpongeza: “Imekuwa ni siku ya furaha kwetu na Serena Williams kwa kuingia katika dunia mpya! Hongera kwa kutegemea kupata mtoto hivi karibuni.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here