SHARE

LONDON, England

MWAMUZI maarufu katika Ligi Kuu England, Mike Dean, amekabidhiwa rungu la kusimamia sheria 17 za soka kati ya Chelsea na Manchester United utakaopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Dean anasifika kwa kugawa kadi katika michezo anayochezesha, lakini pia ni mwamuzi anayesimamia misimamo yake anapokuwa uwanjani.

Katika michezo mitatu iliyopita kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Manchester United walifungwa michezo yote, miwili ilikuwa ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika kwa mabao 4-0 na 1-0 huku mwingine michuano ya Kombe la FA hatua ya robo fainali ulimalizika kwa Chelsea kushinda bao 1-0.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here