SHARE
during the Barclays Premier League match between XXX and XXX at

LONDON, England

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Dele Alli, anajipanga kufanya kazi na wakala mwingine ambaye atahusika katika sekeseke ‘linalopikwa’ kuwa kiungo huyo atasaka timu nyingine majira yajayo ya kiangazi.

Alli hatasaka timu nyingine tu, bali atahitaji timu itakayomlipa mshahara mnono, kitu ambacho kitailazimu Spurs kuvuruga malipo yao ya mshahara kama watataka abaki London.

Uamuzi wa staa huyo wa England kufikiria suala la kuachana na wakala wake wa muda mrefu, Rob Segal, umeziweka timu kubwa za Ulaya mkao wa kula wa kumnasa Alli majira yajayo ya kiangazi.

Segal amefanya kazi na Alli tangu akiwa katika klabu ya MK Dons, lakini mchezaji huyo kwa sasa anataka kubadilisha wakala na makampuni mengine yenye upinzani kwenye masuala ya uwakala yameanza kuvizia tenda.

Alli alisaini mkataba mpya wa miaka sita Septemba mwaka jana na analipwa mshahara wa pauni 60,000 kwa wiki. Lakini, kutokana na kiwango kizuri alichokionesha katika muda wote huo aliotumia kuichezea klabu hiyo, anadhani sasa ni wakati wa kukamata zaidi ya pauni 200,000 kwa wiki.

Wakala huyo mpya atakayepewa tenda, atashughulika katika suala la kuhakikisha mteja wake anapata mshahara mnono kama anavyotaka na Spurs haina budi kumuongezea iwapo wanataka aendelee kuwa mali yao.

Hiyo ni fursa ambayo imeanza kufukuziwa na miamba ya soka Ulaya ambayo inatajwa kumtaka Alli. Timu mbili kubwa za Jiji la Manchester, Chelsea, Real Madrid na Paris Saint-Germain zote zimetajwa kuanza kummendea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here