Home Michezo Kimataifa DELE ALLI HATARINI KUSHUGHULIKIWA NA FIFA

DELE ALLI HATARINI KUSHUGHULIKIWA NA FIFA

386
0
SHARE

LONDON, England

SHIRIKISHO la Soka Duniani, Fifa, limeanza mchakato wa kumshikisha adabu kiungo mshambuliaji wa England, Dele Alli, kutokana na kitendo chake cha kuonesha ishara ya kidole cha kati.

Alli alidai kuwa, ishara hiyo aliyoionesha kwenye mchezo wa baina ya England na Slovakia mapema wiki hii, ilikuwa ni kwa mchezaji mwenzake, Kyle Walker na si kwa mwamuzi Mfaransa, Clement Turpin, kama ilivyodaiwa hapo awali.

Lakini licha ya kujitetea huko, bado kitendo hicho kimetafsiriwa kama ‘tusi’ na Fifa wana nguvu ya kumwadhibu mchezaji huyo.

Aidha, Shirikisho la Soka nchini England (FA) limepewa muda hadi Jumatano kuwasilisha utetezi wao kwa nyota huyo, na wanaamini ushahidi wa TV utawasaidia kudhihirisha kwamba ishara hiyo haikuelekezwa kwa mwamuzi.

Fifa pia huenda wakahitaji maelezo ya Walker kuhusiana na tukio hilo, ambapo kipengele cha 57 cha kanuni ya nidhamu ya FIFA, hakijasema lolote kuhusu mlengwa, ingawa kuwatusi waamuzi wa mchezo kiuhalisia ni jambo litakalochunguzwa kwa umakini zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here