SHARE

MWAMVITA MTANDA

UNAMJUA winga machachari wa Simba, Deo Kanda, aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea TP Mazembe ya nchini DR Congo? Kama ndiyo basi hebu subiri muziki wake katika mechi zijazo uone balaa lake.

Unaambiwa Mcongo huyo ambaye katika maisha yake amekuwa akiota kuichezea Simba na hatimaye ndoto zikafanikiwa, anaona bado hajaifanyia lolote la maana klabu hiyo katika mechi kadhaa alizopata nafasi ya kucheza.

Miungoni mwa mechi hizo ni ile ya tamasha la Simba Day ambapo aliichezea timu hiyo dhidi ya Power Dynamos ya Zambia, na pia kusaidia timu yake hiyo kupata ushindi wa wa mabao 3-1, kisha ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji.

Jana ndiyo siku alipovunja ukimya na kuliambia DIMBA Jumatano katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam kwamba kwasasa ameapa kuipigania timu hiyo kwa nguvu zake zote.

Aliongeza kusema, heshima aliyopewa katika kikosi hicho ni kubwa na yeye atahisi ameitendea haki hadhi hiyo kwa kufunga mabao na pia kuisaidia timu yake kupata ushindi.

Awali kocha mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems, alisema Kanda ni moja ya wachezaji wazuri wanaojituma na kufuata haraka maelekezo yake.

Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa, winga huyo akapewa nafasi pana katika kikosi hicho hasa katika mechi zinazotarajiwa kuchezwa hivi karibuni dhidi ya Azam FC, Ngao ya Jamii, itakayochezwa Jumamosi hii, pia mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji itakayoichezwa kati ya Agosti 23 na 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here