Home Burudani Diamond ampachika mimba Zari, atarajia kupata kidume Desemba

Diamond ampachika mimba Zari, atarajia kupata kidume Desemba

795
0
SHARE

NA KYALAA SEHEYE,

MFALME wa Afro Pop Afrika Mashariki, Nassib Abdul Juma ‘Diamond’, anatarajia kupata mtoto wa pili wa kiume Desemba mwaka huu kutoka kwa mpenzi wake, Africasti wa Kiganda Zarina Hassan, a.k.a Zari the Boss Lady.

Akihojiwa na kituo na Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam kupitia kipindi cha Leo Tena, mfalme huyo asiyepingika katika ulimwengu wa muziki amethibitisha kuwa muda si mrefu atakuwa baba wa watoto wawili.

“Tiffa anatarajia kufikisha mwaka mmoja Agosti 6 mwaka huu na Desemba inshaalah natarajia kupata mtoto wa kiume ambaye jina lake nitalianika hapo baadaye,” alisema Diamond.

Amesisitiza kuwa tangu awe na Zari hajawahi kumsaliti hata siku moja na anampenda sana kwa sababu maneno anayoyasikia kwa wabaya wao amekuwa akiyapuuzia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here