SHARE

NA BEATRICE KAIZA

MENEJA wa mwanamuziki nyota barani Afrika, Diamond Platnumz, Said Fella amesema, wamepeleka maombi serikalini kuomba kupewa eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam kujenga Sanamu ya msanii huyo.

Akizungumza na DIMBA, Fella, alisema,anaiomba Serikali imchukulie Diamond kama mlima wa Kilimanjaro kwa namna anavyoing’arisha Tanzania kimataifa na kuwa kivutio cha utalii.

ëíDiamond kwa sasa ni kivutio cha nchi na tayari tumepeleka maombi Serikali ili kuweza kujenga sanamu maeneo ya Kigogo ili kuweka ukumbusho kutokana na kazi yake ambazo amefanya kuitangaza muziki ndani na nje ya nchi, alisema Fella.

Aliongezea kuwa pia wataomba uongozi wa Mkoani Kigoma kujenga sanamu ili kuweza kuingiza kipato kwa Serikali kama watu wakipiga picha kwenye sanamu na hela itasaidia kwenye mambo mabalimbali ya kuijenga nchi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here