Home Habari DIDA AIBUKIA MAZOEZINI YANGA

DIDA AIBUKIA MAZOEZINI YANGA

521
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE


KIPA namba moja wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’, amerejea kimyakimya na kujiunga kwenye mazoezi na wenzake, licha ya kuaga kwenda nchini Afrika Kusini kutafuta bahati yake.

Dida ameonekana kwenye mazoezi ya Yanga tangu wiki hii ianze ambapo Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa, amethibitisha hilo huku akidai kwamba hawajakaa meza moja na kuzungumza naye kuhusu mkataba mpya.

“Alituaga kwamba anakwenda Afrika Kusini, tukamruhusu lakini sasa amerejea na ameanza mazoezi na wenzake, ila bado hatujazungumza naye chochote kama amefaulu majaribio yake ama la,” alisema.

Awali baada ya kipa huyo kudai kwamba anakwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio na timu ambayo hata hivyo hakuiweka wazi, zilienea taarifa kwamba Singida United wanamfukuzia lakini sasa mwenyewe ameamua kujisalimisha Yanga.

Taarifa nyingine kutoka Yanga zinadai kuwa Dida amefuzu majaribio yake ambapo baada ya taarifa hizo kuvuja, DIMBA Jumatano lilimtafuta kipa huyo bila mafanikio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here