Home Uchambuzi DILUNGA ANAVYOLIAMSHA VITA YA NAMBA SIMBA

DILUNGA ANAVYOLIAMSHA VITA YA NAMBA SIMBA

7610
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

KIWANGO cha juu kilichoonyeshwa mwishoni mwa wiki na kiungo wa Simba, Hassan Dilunga mchezo wa Ngao wa Jamii uliowakutanisha na Mtibwa Sugar ni dalili za mapambano endelevu ya  kuwania nafasi kikosi hapo.

Ingizo hilo jipya kutoka Mtibwa alikuwa chachu ya Simba ya kocha Patrick Aussems kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kumfanya mnyama kutetea taji hilo kwa mara nyingine.

Ulikuwa ni mchezo wa pili kwa nyota kuonyesha namna ya kutumia nafasi mchezaji unapoaminiwa na kocha kutoka kundi kubwa la wachezaji ikiwa ni baada ya kufanya hivyo  mapema Agosti 8 dhidi Asante Katoko ya Ghana(Simba Day).

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Mwanza,Dilunga alikuwa kikwazo kwa timu yake hiyo ya zamani hasa eneo la kiungo alipokuwa anacheza sambamba na Jonas Mkude pamoja na James Kotei.

Mbali na kutoa pasi rula iliyomkuta Meddie Kagere na kupiga shuti la pili lililowagonga  akina Hassan Isihaka na kutinga wavuni, lakini pia Dilunga alikuwa kiunganishi kikubwa cha timu.

Ni yeye ambaye  alikuwa amepiga mashuti mengi langoni kwa Mtibwa Sugar akifanya hivyo mara nne, mawili yakilenga lango, moja likipaa juu, na lingine likipita sentimita chache mlingoti.

Lakini pia akikimbia umbali mrefu uwanjani akihaha kukaba, akitimiza jukumu la kupiga pasi nyingi sahihi zilizofika kwa walengwa ‘key pass’,pass accurance,complete pass’ vyote vilionekana mguuni kwake. Jibu lake ni kwamba huyu ni kiungo wa kisasa aliyekamilika.

Hata hivyo katika makazi hayo mapya anazungukwa na mafundi wengine wanaocheza eneo hilo,kitendo kinacholifanya benchi la ufundi kuumiza zaidi kichwa kuitisha glasi ya maji ya kunywa wakati wa upangaji wa kikosi cha kwanza.

Safi hiyo ya kiungo iliongozwa na Mkude aliyecheza michezo mingi zaidi msimu uliopita,mbali na kina Mzamiru Yassin, Kotei, Haruna Niyonzima, Said Ndemla, pia kuna ingizo lingine Mzambia Cleatus Chama.

Orodha hiyo ya viungo ambayo kila mmoja anajukulina uwezo wake kuipigania timu jambo, jipya linalotarajiwa na mashabiki ni namna uwajibikaji mchezaji mwenyewe katika mazoezi aonekane mchezo husika.

Dilunga na Chama soka lao linaonekana kushabihiana wanakaba, wanapokonya, wanapiga pasi nyingi sahihi zikiwamo za kwenda kwa Okwi,Kagere na Bocco, lakini pia jukumu mama la kuunganisha timu.

Hiyo ni tofauti na Mkude ambaye ni mzuri sana kuwalinda mabeki wake  akitumia nguvu na akili kusambaza mipira,lakini ni mara chache kumuona amesogea juu zaidi huenda kuhofia kasi kwani si mtu wa mbio.

Ndemla, Mzamiru ni wazuri wakiwa na mpira mguuni kuufanya wanavyotaka wakiuamuru mwelekeo watakao kwa usahihi  wa uwanja pamoja na jicho la kuwatungua makipa, lakini suala la kukaba ndipo wanapopwaya.

Wakati safu ya kiungo ikiwa moto, idara nyingine ni wachana nyavu, Emmanuel Okwi,Shiza Kichuya, Meddie Kagere,John Bocco,Adam Salamba,Marcel Kaheza na Mohamed Rashid.

Mfungaji bora wa msimu uliopita, Okwi anaonekana kuwa na nafasi kubwa kuendelea kutesa eneo hilo mabao matano mechi tano za kirafiki ni kishawishi tosha kwenda benchi la ufundi.

Pacha wake Bocco walitengeneza kombinesheni kali msimu uliopita akiwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa usahihi, kichwa pia kikifanya kazi kutumia vema krosi na mpira mirefu. Kazi anayo Mbelgiji Aussems.

Meddie Kagere  mwenye nguvu miguuni na mbio aliyemzidi maarifa Isihaka sambamba na kipa, Benedickt Tinocco pia ana nafasi kubwa ndani ya kikosi cha kwanza kati yake na kina Okwi na Bocco.

Salamba mwenye umbo kubwa ambaye amekuwa akitokea benchi mechi kadhaa za kirafiki, nyuma yake anapambana na kina Kaheza na Rashid huku Kichuya anayetokea pembeni wakati ana nafasi kubwa kuendelea king’ang’anizi upande huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here