SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongofleva Abdulaziz Chande maarufu ‘Dogo Janja’ ametumia siku ya sherehe ya kuzaliwa ya mpenzi wake kumvisha pete ya uchumba.
Dogo Janja ambaye aliwahi kufunga ndoa na staa wa Bongomovie Irene Uwoya kisha kuachana, kwa sasa yupo kwenye dimbwi zito la mahaba na mpenzi wake mpya anajulikana kwa jina la QueenLinah.
Akizungumza na DIMBA Jumatano, Dogo Janja alisema,hajakurupuka kufanya maamuzi hayo kwani ni wazi kwa sasa anataka kuingia rasmi kwenye ndoa baada ya yeye na mpenzi wake kuridhiana.
“Linah amenitoa mbali, ni mwanamke wa mfano, anajua nini mwanamke anapaswa kufanya, nadhani huu ni wakati wangu sahihi wa kutimiza kile nilichomuahidi, hii ni taratibu ya awali nyingine zinakuja”alisema Dogo Janja.
Aliongeza uamuzi wa kumvisha mrembo huyo pete umekuja kwa wakati kwani alitamani mwaka huu kufanya mambo makubwa zaidi ikiwemo suala zima la ndoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here