SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

DONALD Ngoma, yule mshambuliaji wa Yanga, amejipambanua kuwa anamwamini zaidi Mwenyezi Mungu, kwani kila akiweka ‘posti’ kwenye mtandao wake wa Facebook, lazima amkumbuke Muumba wake huyo.

Katika posti zake za hivi karibuni, straika huyo Mzimbabwe, amekuwa akiweka maneno ya kumtukuza Mungu, hiyo ikiashiria kuwa anajua huyo ndiye muweza wa yote.

Moja ya posti zake za hivi karibuni ni ile aliyoandika: “Roho wa Mungu anakaa juu yake”, ambapo ujumbe huo ameutuma Aprili 27, mwaka huu, yaani Alhamis iliyopita.

Ujumbe mwingine ambao ameutuma Ijumaa ya wiki hii unasema: “Mwamba ulioko mbele yako, hauwezi kuushinda ule wa Mungu ulioko maishani mwako.”

Ngoma ambaye ni straika wa kutumainiwa wa Yanga, bado anasumbuliwa na majeraha ya mguu na leo pia anatarajiwa kuukosa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC ya Mwanza, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here