SHARE

MANCHESTER, England

MSHINDI mara tatu wa taji la Ligi Kuu England, Jose Mourinho, amejiunga na kituo cha Sky Sports, akiwa sehemu ya wachambuzi wa soka msimu huu.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester United ataanza kazi hiyo leo, kwa kuchambua mchezo ambao utazikutanisha timu zake hizo za zamani, pia mechi nyingine kati ya Newcastle United na Arsenal ambayo itachezwa mapema.

Tangu afukuzwe na Manchester United Desemba mwaka jana, Mourinho bado hajafanikiwa kupata timu ya kuiongoza huku taarifa zikidai, hivi karibuni aligomea dili la kujiunga na klabu moja ya nchini China.

“Ligi Kuu England ni ligi bora na muhimu kwangu, inakuhitaji utumie nguvu kubwa kupata matokeo, inakufanya uiangalie mara kwa mara, nafurahi kuwa sehemu ya wachambuzi wa kituo cha Sky Sport,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here