Home Burudani DUH! UWOYA ATAKA MIL   25/- KOLABO NA DOGO JANJA

DUH! UWOYA ATAKA MIL   25/- KOLABO NA DOGO JANJA

7468
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE


 

STAA wa filamu nchini, Irene Uwoya, amesema endapo mumewe ambaye ni msanii wa muziki wa     kizazi kipya, Abdulkarim  Chande ‘Dogo Janja’, atahitaji kupiga naye kolabo ni lazima avunje benki kwa kumpa kiasi kisichopungua Sh milioni 25.

Akizungumza na    DIMBA Jumatano, Dogo Janja alisema    amekuwa na mawazo ya kumshirikisha mkewe kwenye kazi zake, hivyo ameanza harakati za kusaka fedha ya kumlipa.

“Hii ni kazi kama nyingine..mbali na ukaribu wetu lakini linapokuja suala la kazi basi tunakuwa makini..hata yeye akinihitaji kwenye kazi zake za filamu nitampa masharti yangu,  ni fedha kubwa lakini nitaitafuta na kumlipa ili afanye kazi ninayotaka,” alisema Dogo Janja.

Aliongeza kuwa mkewe amekuwa akimsapoti sana katika shughuli zake za kimuziki na hataona tabu kumlipa kiasi chochote cha fedha atakachohitaji kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here