Home Burudani DULLY SYKES: KUWAPATANISHA DIAMOND, ALLY KIBA NI KUPOTEZA WAKATI

DULLY SYKES: KUWAPATANISHA DIAMOND, ALLY KIBA NI KUPOTEZA WAKATI

530
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE,

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, ‘Prince Dully Sykes’, amesema ikifika muda wa kuwapatanisha nyota wa muziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ na Ally Kiba, atafanya hivyo lakini kwa sasa hivi ni kupoteza wakati.

Diamond na Ally Kiba wamekuwa na bifu la muda mrefu ambalo mpaka sasa hakuna ambaye ameweza kuwapatanisha huku chanzo kikidaiwa kuchochewa na mashabiki wa kila upande wa wasanii hao.

Dully alisema kuwapatanisha mastaa hao kwa sasa kwa upande wake ni kama kutwanga maji kwenye kinu kwa sababu umri wao na bifu zao zinaendana hivyo ikifika muda unaofaa atakaa na kila mmoja na kuondoa tofauti zao.

“Nikisema nichukue nafasi yangu kama kaka yao kuwapatanisha nadhani nitakuwa napoteza muda kwani umri wao wa ujana unawasukuma kufanya hivyo, ngoja niwaache kwanza lakini tatizo lao linachochewa na mashabiki wa kambi hizo mbili,” alisema Dully.

Alisema anachofurahi kwa sasa kutoka kwao ni kuona bado kila mmoja anafanya vizuri kupitia kazi zake na wameendelea kuwa vipenzi kwa mashabiki wao na ugomvi wao haujaweza kuwaathiri kwa chochote mpaka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here