SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MKALI wa ngoma ya ‘Chovya’, Dyana Nyange, amefunguka na kusema kwa sasa ndoto zake ni kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa, kama Yemi Alade, ili kupenyeza muziki wa Tanzania nje ya mipaka ya Afrika Mashariki.

Akizungumza na DIMBA, Dyana alisema tayari ameanza kusogelea soko la kimataifa, ambapo hivi karibuni amefanya ngoma nyingine mpya na mtayarishaji wa muziki kutoka Afrika Kusini aitwaye Captain Blue na kazi hiyo itaanza kuruka hewani hivi karibuni.

“Nadhani sasa ni wakati wangu wa kufanya kazi kimataifa zaidi na tayari nimeanza baada ya kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki Afrika Kusini, pia nipo kwenye mipangilio ya kuwashirikisha mastaa wakubwa kama kina Yemi Alade na wengine, lengo ni kupanua zaidi kazi zangu,” alisema Dyana.

Alisema Chovya ni moja ya kazi ambazo zimemuongezea chati kwa siku za hivi karibuni na kuifunika ile ngoma yake iitwayo ‘Komela’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here